Ayubu 25:1-6
Swahili Union Version (SUV)
Bildadi anazungumzia mamlaka ya Mungu
Swahili Union Version. Bible Society of East Africa.
1Ndipo Bildadi, Mshuhi, akajibu, na kusema,
2Enzi na hofu zi pamoja naye; Hufanya amani katika mahali pake palipoinuka.
3Je! Majeshi yake yahesabika? Ni nani asiyetokewa na mwanga wake?
4Basi mtu awezaje kuwa na haki mbele ya Mungu? Au awezaje kuwa safi aliyezaliwa na mwanamke?
5Tazama, hata mwezi hauangazi, Wala nyota si safi machoni pake;
6Siuze mtu, aliye mdudu! Na mwanadamu, ambaye ni buu!