Zaburi 100:1-5
Swahili Union Version (SUV)
1Mfanyieni Bwana shangwe, dunia yote;
2Mtumikieni Bwana kwa furaha; Njoni mbele zake kwa kuimba;
3Jueni kwamba Bwana ndiye Mungu; Ndiye aliyetuumba na sisi tu watu wake; Tu watu wake, na kondoo wa malisho yake.
4Ingieni malangoni mwake kwa kushukuru; Nyuani mwake kwa kusifu; Mshukuruni, lihimidini jina lake;
5Kwa kuwa Bwana ndiye mwema; Rehema zake ni za milele; Na uaminifu wake vizazi na vizazi.