Zaburi 120:1-7

Swahili Union Version (SUV)

Mzalmi anamwomba Mungu akomoe dhuluma. Anatazama amani lakini akilenga vita.

Swahili Union Version. Bible Society of East Africa.

1Katika shida yangu nalimlilia Bwana Naye akaniitikia.

2Ee Bwana, uiponye nafsi yangu Na midomo ya uongo na ulimi wa hila.

3Akupe nini, akuzidishie nini, Ewe ulimi wenye hila?

4Mishale ya mtu hodari iliyochongoka, Pamoja na makaa ya mretemu.

5Ole wangu mimi! Kwa kuwa nimekaa katika Mesheki; Na kufanya maskani yangu Katikati ya hema za Kedari.

6Nafsi yangu imekaa siku nyingi, Pamoja naye aichukiaye amani.

7Mimi ni wa amani; Bali ninenapo, wao huelekea vita.