Zaburi 123:1-4
Swahili Union Version (SUV)
Mwokozi anamwomba Mungu atuonee huruma. Tunahitaji huruma kutokana na dharau na kelele.
Swahili Union Version. Bible Society of East Africa.
1Nimekuinulia macho yangu, Wewe uketiye mbinguni.
2Kama vile macho ya watumishi Kwa mkono wa bwana zao Kama macho ya mjakazi Kwa mkono wa bibi yake; Hivyo macho yetu humwelekea Bwana, Mungu wetu, Hata atakapoturehemu.
3Uturehemu, Ee Bwana, uturehemu sisi, Kwa maana tumeshiba dharau.
4Nafsi zetu zimeshiba mzaha wa wenye raha, Na dharau ya wenye kiburi.