Zaburi 127:1-5

Swahili Union Version (SUV)

Mwanadamu anahitaji kuwa chini ya Mungu. Mafanikio yanatokana na neema yake.

Swahili Union Version. Bible Society of East Africa.

1Bwana asipoijenga nyumba Waijengao wafanya kazi bure. Bwana asipoulinda mji Yeye aulindaye akesha bure.

2Kazi yenu ni bure, mnaoamka mapema, Na kukawia kwenda kulala, Na kula chakula cha taabu; Yeye humpa mpenzi wake usingizi.

3Tazama, wana ndio urithi wa Bwana, Uzao wa tumbo ni thawabu.

4Kama mishale mkononi mwa shujaa, Ndivyo walivyo wana wa ujanani.

5Heri mtu yule Aliyelijaza podo lake hivyo. Naam, hawataona aibu Wanaposema na adui langoni.