Zaburi 134:1-3

Swahili Union Version (SUV)

Watumishi wa Bwana wanahimidiwa kumwabudu. Bwana huwabariki.

Swahili Union Version. Bible Society of East Africa.

1Tazama, enyi watumishi wa Bwana, Mhimidini Bwana, nyote pia. Ninyi mnaosimama usiku Katika nyumba ya Bwana.

2Painulieni patakatifu mikono yenu, Na kumhimidi Bwana.

3Bwana akubariki toka Sayuni, Aliyezifanya mbingu na nchi.