Zaburi 29:1-11

Swahili Union Version (SUV)

Zaburi 29 inasifu nguvu ya Bwana. Inaangazia utawala wake juu ya ulimwengu.

Swahili Union Version. Bible Society of East Africa.

1Mpeni Bwana, enyi wana wa Mungu, Mpeni Bwana utukufu na nguvu;

2Mpeni Bwana utukufu wa jina lake; Mwabuduni Bwana kwa uzuri wa utakatifu.

3Sauti ya Bwana i juu ya maji; Mungu wa utukufu alipiga radi; Bwana yu juu ya maji mengi.

4Sauti ya Bwana ina nguvu; Sauti ya Bwana ina adhama;

5Sauti ya Bwana yaivunja mierezi; Naam, Bwana aivunjavunja mierezi ya Lebanoni;

6Airusharusha kama ndama wa ng'ombe; Lebanoni na Sirioni kama mwananyati.

7Sauti ya Bwana yaipasua miali ya moto;

8Sauti ya Bwana yalitetemesha jangwa; Bwana alitetemesha jangwa la Kadeshi.

9Sauti ya Bwana yawazalisha ayala, Na kuifichua misitu; Na ndani ya hekalu lake Wanasema wote, Utukufu.

10Bwana aliketi juu ya Gharika; Naam, Bwana ameketi hali ya mfalme milele.

11Bwana atawapa watu wake nguvu; Bwana atawabariki watu wake kwa amani.