Zaburi 54:1-7
Swahili Union Version (SUV)
Daudi anamwomba Mungu kusaidia dhidi ya adui. Anamshukuru Mungu kwa kuokoa.
Swahili Union Version. Bible Society of East Africa.
1Ee Mungu, kwa jina lako uniokoe, Na kwa uweza wako unifanyie hukumu.
2Ee Mungu, uyasikie maombi yangu, Uyasikilize maneno ya kinywa changu.
3Kwa maana wageni wamenishambulia; Watu watishao wananitafuta nafsi yangu; Hawakumweka Mungu mbele yao.
4Tazama, Mungu ndiye anayenisaidia; Bwana ndiye anayenitegemeza nafsi yangu.
5Atawarudishia adui zangu ubaya wao; Uwaangamize kwa uaminifu wako.
6Kwa ukunjufu wa moyo nitakutolea dhabihu; Ee Bwana, nitalishukuru jina lako, maana ni jema.
7Kwa kuwa limeniokoa na kila taabu; Na jicho langu limeridhika Kwa kuwatazama adui zangu.